TANGAZO RASMI: WALIMU NA KADA MBALIMBALI WALIOTEULIWA KUANZA KAZI – 22 MACHI 2025,Walimu walioitwa kazini
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetoa orodha rasmi ya waombaji kazi waliofaulu usaili uliofanyika kati ya tarehe 4 Aprili 2024 na 24 Februari 2025. Tangazo hili linajumuisha majina ya waombaji waliofaulu pamoja na wale waliokuwepo kwenye kanzidata (database) kwa kada mbalimbali, ambao sasa wamepangiwa vituo vya kazi.
Maelekezo Muhimu kwa Waliofaulu
Uchukuaji wa Barua za Kupangiwa Kituo cha Kazi:
-
Waliofaulu wanapaswa kuchukua barua zao za kupangiwa vituo vya kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Jengo la Dkt. Asha Rose Migiro, ndani ya siku saba (7) kutoka tarehe ya tangazo hili.
-
Baada ya muda huo, barua ambazo hazitachukuliwa zitatumwa kupitia anuani za Posta.
Kuripoti Katika Vituo vya Kazi:
-
Waajiriwa wote wanapaswa kuripoti kwa waajiri wao ndani ya muda uliobainishwa kwenye barua zao za ajira.
-
Lazima wawe na vyeti halisi vya taaluma (kuanzia kidato cha nne na kuendelea) kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupokea barua rasmi ya ajira.
Hitaji la Kitambulisho:
Wanaochukua barua za kupangiwa kazi lazima wawe na kitambulisho halali cha utambulisho, kimoja kati ya vifuatavyo:
-
Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
-
Pasipoti
-
Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi
-
Kitambulisho cha Mpiga Kura
-
Leseni ya Udereva
Vipi Kama Jina Lako Halipo?
Ikiwa jina lako halipo kwenye orodha hii, tafadhali tambua kuwa hukufaulu katika mchakato huu wa ajira. Usikate tamaa! Unahimizwa kuendelea kuomba nafasi nyingine za ajira zitakapotangazwa.
Pakua Orodha Kamili ya Majina
Ili kuthibitisha kama jina lako limo kwenye orodha ya walioajiriwa, pakua tangazo rasmi katika kiungo kilicho hapa chini:
Endelea kufuatilia matangazo rasmi ya ajira kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa taarifa zaidi. Hongera kwa wote waliofaulu!