Nafasi za kazi Idara ya Uhamiaji Tanzania, Tangazo la Nafasi za Ajira Mpya: Idara ya Uhamiaji Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Idara ya Uhamiaji
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anatangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa za kujiunga na Idara ya Uhamiaji kama Askari wa Uhamiaji. Hii ni fursa muhimu kwa wale wanaotamani kutumikia Taifa na kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi kupitia huduma za uhamiaji.
Sifa za Mwombaji
Ili kufuzu kwa nafasi hizi, mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe hana ajira na hajawahi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali.
- Awe na cheti halali cha kuzaliwa.
- Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya Utambulisho kutoka NIDA.
- Awe na afya njema ya mwili na akili.
- Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
- Asiwe na rekodi ya uhalifu au kuhusika katika vitendo vya jinai.
- Asiwe na michoro au alama za kudumu mwilini (tatoo).
- Awe hajaoa au kuolewa, na asiwe na watoto.
- Umri wa Mwombaji:
- Elimu ya Kidato cha Nne: Miaka 18–22.
- Elimu ya Kidato cha Sita au Stashahada: Miaka 18–25.
- Elimu ya Shahada au Stashahada ya Juu: Miaka 18–30.
- Awe tayari kufanya kazi katika maeneo yoyote nchini Tanzania.
- Awe tayari kugharamia mchakato mzima wa maombi na uteuzi wa ajira.
Vipaumbele vya Maombi
Waombaji wenye taaluma katika fani zifuatazo watapewa kipaumbele:
- Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano wa Umma, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa rasmi), Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa Vifaa vya Kupooza Hewa (AC), Usalama wa Mtandao (Cyber Security), Bendi ya Miziki ya Brass, na Uchapaji (Printing).
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote ya ajira yanapaswa kuwasilishwa kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji: https://www.immigration.go.tz.
Muda wa Kutuma Maombi: Kuanzia tarehe 29 Novemba, 2024 hadi tarehe 13 Disemba, 2024.
Mwombaji anatakiwa kuambatisha nyaraka zifuatazo katika mfumo wa PDF (kila moja isizidi 300KB):
- Picha ya pasipoti (passport size) ya hivi karibuni (mfumo wa jpg/png, isiwe zaidi ya 300KB).
- Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono.
- Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au Mkuu wa Kambi (kwa walio JKT/JKU).
- Cheti cha kuzaliwa.
- Kitambulisho cha Taifa au Namba ya NIDA.
- Vyeti vya elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Kidato cha Sita).
- Vyeti vya taaluma kwa ngazi ya Stashahada, Stashahada ya Juu, au Shahada vilivyohakikiwa.
- Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili rasmi.
- Wasifu wa Mwombaji (CV).
Tahadhari Muhimu
- Maombi yote yatapokelewa kwa utaratibu uliowekwa hapo juu pekee.
- Nyaraka za kughushi zitasababisha hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
- Epuka matapeli wanaodai pesa au rushwa kwa ahadi ya kusaidia kupata ajira.
Imetolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji, Dodoma
Tarehe: 29 Novemba, 2024
Bonyeza hapa kuona PDF; TANGAZO-LA-AJIRA-MPYA-2024-1
Leave a Reply