Ajira Mpya Idara ya Uhamiaji Tanzania 2024/2025

Ajira Mpya Idara ya Uhamiaji Tanzania
Ajira Mpya Idara ya Uhamiaji Tanzania

Ajira Mpya Idara ya Uhamiaji Tanzania, Nafasi za  kazi Idara ya Uhamiaji Tanzania, Tangazo la Nafasi za Ajira Mpya: Idara ya Uhamiaji Tanzania

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Idara ya Uhamiaji

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana wa Kitanzania fursa za ajira kwa nafasi za Askari wa Uhamiaji. Nafasi hizi ni kwa wale waliokidhi vigezo vilivyotajwa na wanaotamani kutumikia Taifa kupitia Idara ya Uhamiaji.

Sifa za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe hana ajira na hajawahi kuajiriwa katika taasisi yoyote ya Serikali.
  3. Awe na cheti halali cha kuzaliwa.
  4. Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya Utambulisho kutoka NIDA.
  5. Awe na afya njema ya mwili na akili.
  6. Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
  7. Asiwe na rekodi ya uhalifu au kuhusika katika vitendo vya jinai.
  8. Asiwe na michoro au alama za kudumu mwilini (tatoo).
  9. Awe hajaoa wala kuolewa, na asiwe na watoto.
  10. Umri wa Mwombaji:
  • Elimu ya Kidato cha Nne: Miaka 18–22.
  • Elimu ya Kidato cha Sita au Stashahada: Miaka 18–25.
  • Elimu ya Shahada au Stashahada ya Juu: Miaka 18–30.
  1. Awe tayari kufanya kazi katika maeneo yoyote nchini Tanzania.
  2. Awe tayari kugharamia mchakato mzima wa maombi na uteuzi wa ajira.

Vipaumbele vya Maombi

Waombaji walio na taaluma katika fani zifuatazo watapewa kipaumbele:

  • Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano wa Umma, TEHAMA, Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi (waliosajiliwa rasmi), Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa Magari, Ufundi wa Vifaa vya Kupooza Hewa (AC), Usalama wa Mtandao (Cyber Security), Bendi ya Miziki ya Brass, na Uchapaji (Printing).

Jinsi ya Kutuma Maombi

Maombi yote ya ajira yanapaswa kuwasilishwa kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji: https://www.immigration.go.tz.

Muda wa Kutuma Maombi: Kuanzia tarehe 29 Novemba, 2024, hadi tarehe 13 Disemba, 2024.

Mwombaji anatakiwa kuambatisha nyaraka zifuatazo kwa mfumo wa PDF (kila moja isizidi 300KB):

  • Picha ya pasipoti (passport size) ya hivi karibuni (mfumo wa jpg/png, isiwe zaidi ya 300KB).
  • Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono.
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa au Mkuu wa Kambi (kwa walio JKT/JKU).
  • Cheti cha kuzaliwa.
  • Kitambulisho cha Taifa au Namba ya NIDA.
  • Vyeti vya elimu ya sekondari (Kidato cha Nne na Kidato cha Sita).
  • Vyeti vya taaluma kwa ngazi ya Stashahada, Stashahada ya Juu, au Shahada vilivyohakikiwa.
  • Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili rasmi.
  • Wasifu wa Mwombaji (CV).

Tahadhari Muhimu

  1. Maombi yote yapokelewa kwa utaratibu uliowekwa hapo juu pekee.
  2. Nyaraka za kughushi zitasababisha hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
  3. Epuka matapeli wanaodai pesa au rushwa kwa ahadi ya kusaidia kupata ajira.

Imetolewa na:
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Makao Makuu ya Uhamiaji, Dodoma
Tarehe: 29 Novemba, 2024

Angalia PDF hapa; TANGAZO-LA-AJIRA-MPYA-2024-1